Narendra Modi na Rais Tinubuwakutana mjini Abuja, Nigeria
17 Novemba 2024Mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ni kituo cha kwanza katika ziara ambayo itampeleka Waziri Mkuu wa India kwenye mkutano wa G20 nchini Brazil, na Guyana. Ziara hiyo inafanyika huku kukiwa na msukumo ulioanzishwa na India na Nigeria kuhusu uwakilishi wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Soma Pia: Benki ya Dunia yaiidhinishia Nigeria dola bilioni 1.57
Wanachama watano wa kudumu wa baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa ambao ni Marekani, Urusi, China, Ufaransa na Uingereza kila mmoja ana kura ya turufu yenye nguvu. Katika miaka ya hivi karibuni, wafuasi wa sera ya kugawana mamlaka kwa usawa wamekuwa wakishinikiza kuongezwa nchi za Kiafrika, Asia na Amerika ya Kusini kwenye orodha ya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.