NEW YORK: Jallow wa Gambia ateuliwa kwa awamu ya pili
15 Septemba 2007Matangazo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limemchagua tena Hassan Bubacar Jallow wa Gambia kama mwendesha mashtaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu wa vita vya Rwanda.Awamu ya pili ya miaka minne inaanza leo Jumamosi, lakini Jallow huenda asimalize kipindi hicho ikiwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuhusu Rwanda itamaliza kazi zake mwaka 2010,kama ilivyopangwa.
Mahakama hiyo iliundwa miaka 13 iliyopita kuwashtaki washukiwa wakuu,kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.Zaidi ya watu 800,000 waliuawa na Wahutu wa itikadi kali.Wengi waliouawa walikuwa wa kabila la wachache la Kitutsi na pia Wahutu wa sera za wastani.