Nzige wa jangwani wamevamia baadhi ya maeneo nchini Kenya tangu mwezi Disemba. Nzige hao wamesababisha uharibifu mkubwa kwa mimea na miti. Miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa ni Mandera, Marsabit na Isiolo. Wataalam wa Mazingira wanasema mabadiliko ya tabia nchi ndiyo sababu kuu ya uvamizi wa nzige hao. Makala ya Mtu na Mazingira inaangazia suala hilo. Muandaaji na msimulizi ni Michael Kwena.