Ongezeko la joto duniani lilipindukia muongo uliopita.
8 Juni 2023Ripoti hiyo imetolewa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira unaoendelea mjini Bonn. Ripoti hiyo iliyochapishwa leo katika jarida la data za mfumo wa sayansi ya dunia, inaonesha kuwa shughuli za binadamu zinasababisha joto kupanda kwa nyuzi 0.2 za Celsius kila baada ya muongo mmoja.
Soma Zaidi: Kiwango cha joto duniani kuongezeka kwa nyuzi 1.5 katika miaka 5 ijayo
Katika Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi, COP28 utakaofanyika kati ya Novemba 30 na Desemba 12 mwaka huu, ulimwengu utatathmini hatua inazozichukua, na kuzilinganisha na malengo iliyojiwekea mjini Paris mwaka 2015. Malengo hayo ni kubakisha ongezeko la joto katika kiwango cha asilimia 1.5 juu ya hali ya kabla ya mapinduzi ya viwanda, la sivyo dunia itakumbwa na majanga.