Polisi 200 zaidi wa Kenya waelekea Haiti
16 Julai 2024Maafisa wengine 200 wa polisi wa Kenya waliondoka Jumatatu usiku kuelekea Haiti, chini ya mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unaolenga kumaliza ghasia za magenge ya wahalifu katika taifa hilo la Caribbean.
Soma pia: Kikosi cha kulinda amani Haiti chaahidi kuleta utulivu
Taarifa hii imetolea na maafisa wakuu wa polisi wa Kenya waliosema kuwa zoezi hilo litaendelea hadi kufikia idadi ya polisi 1,000. Kundi la kwanza la maafisa 400 waliwasili Haiti mwezi Juni.
Soma pia: Kikosi cha Kenya chajitolea dhidi ya magenge Haiti
Kwa miaka mingi Haiti imekuwa ikikabiliwa na uhalifu wa magenge wa watu wenye silaha ambayo kwa sasa yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu wa Port-au-Prince na pia barabara kuu katika nchi hiyo maskini ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa pia na misukosuko ya kisiasa.